• September 16, 2024
  • Last Update July 1, 2024 6:17 PM
  • Nairobi

Mradi wa ujenzi wa visima katika shule kuanza

Mradi wa ujenzi wa visima katika shule kuanza

Molo,

Jumatano Aprili 17, 2024

KNA na Emily Kadzo

Waziri wa Maji, Zachariah Njeru, amesema kwamba uchimbaji wa visima katika shule, utaanza hivi karibuni ili kuwawezesha wanafunzi kushughulika na masomo yao kikamilifu.

Njeru alisema kuwa ukosefu wa maji katika shule husababisha wanafunzi kupoteza muda mwingi kwenda kutafuta maji badala ya kusoma au hata kulazimika kubeba maji kutoka nyumbani na hivyo basi itakuwa bora iwapo watoto watapata maji karibu ili waimarishe usafi na hata kupata muda wa kutosha kwa masomo.

Waziri aliendelea kusema kuwa uhaba wa maji katika shule za serikali umesababishwa na kukatiwa kwa huduma za maji kutokana na kuongezeka kwa bili za maji na hivyo basi serikali ikachukua hatua hii ya kuchimba visima shuleni na sio tu kufaidi wanafunzi bali hata majirani wa shule hizi wanaohitaji bidhaa hii muhimu.

Hata hivyo, aliwaomba wale watakaonufaika na mpango huu kuhakikisha kuwa maji yanatumika vyema na kuendelea kudumisha usafi wakati wote.

Njeru alikuwa akizungumza katika eneo la Kuresoi Kaskazini alikokuwa amefika kwa mazishi ya familia ya watu saba walioangamia katika ajali ya barabarani eneo la Salama katika barabara kuu ya Nairobi-Mombasa wiki mbili zilizopita.

Hisani; KNA

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *