• May 27, 2024
  • Last Update May 26, 2024 7:22 PM
  • Nairobi

Vijana waombwa kujisajili ili wawe katika mpango wa ajira

Vijana waombwa kujisajili ili wawe katika mpango wa ajira

Molo,

Jumatano Aprili 17, 2024

KNA na Emily Kadzo

Naibu Kamishna wa eneo la Kuresoi Kaskazini, Albanas Ndiso amewaomba vijana kutokosa katika mpango wa kujisajili aina ya ujuzi walionao ili wapate fursa mwafaka ya kupata ajira na kuweza kujikimu kimaisha.

Akizungumza katika eneo lake, Ndiso alisema kuwa mpango huu wa kitaifa wa serikali unanuia kuwapatia vijana fursa ya kupata ajira mahala popote bila aina yoyote ya ubaguzi.

Hadi kufikia sasa, vijana 462 wamejisajili na wanatarajia wengi zaidi watajitokeza na hivyo basi kuwezesha serikali kupata idadi kamili ya vijana na kuweka mikakati kabambe ya kutoa ajira.

Aidha, aliwasihi wale wasio na ujuzi kujiunga na shule za kiufundi ili wapate mafunzo yanayostahili na kuweza kujisajili katika jukwaa hili mtandaoni.

Ndiso aliendelea kusema kuwa yeyote anayehitaji kujisajili apate anwani ya mtandaoni (link) kutoka kwa machifu wa maeneo wanayotoka na kuweka maagizo kama inavyostahili.

Hisani; KNA

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *